CoNept Afya Consultation

CoNept Afya Consultation

Friday, September 13, 2013

Biashara ya mtandao

Habari msomaji, Leo ningependa tuzungumze kidogo kuhusu biashara ya mtandao Biashara ya mtandao ni biashara iliyoingiaulimwenguni miaka mingi iliyopita inayotumia watu katika kuitangaza bidhaa za kampuni fulani Biashara hii hapa kwetu nchini watu wengi wamekuwa wakihofia kuifanya kwasababu mbali mbali zikiwemo ni biashara ya kimachinga, wasiosoma ndio wanaifanya, na haiwezekani benefit zinazokuwa zikielezwa humo ndani kupatikana, biashara ya kitapeli biashara ya freemason na mengineyo mengi. Lakini je haya yote ni imani ya kweli? Kwa kuwa tunakuwa tunakosa maarifa ndio maana ni ngumu sana kumueleza mtu akaelewa faida na hasara ya biashara hii na pia waliotangulia kuifanya biashara hii walikosa maarifa wakaifanya ikawa na sifa hizo Biashara ya mtandao ni biashara kama biashara nyingine na ni ajira kama mtu mwingine anavyoajiriwa kasoro huku hamna atakayekuwekea ratiba ya kufanya kazi wala atakayekuongoza kufanya kazi ina maana wewe ni boss na wewe ni mwajiriwa na wewe ndio kila kitu,,,,,, hapa ndio mtanzania anashindwa kufanya biashara hii kwasababu anapenda kutumwa na kupelekeshwa, anapenda akafanya sales kwa wahindi alipwe laki nane kwa mwenzi huku kamuingizia mwindi milioni mia kwa mwezi haoni kama anatumika wala haoni kama anamtajirisha mtu as long anaitwa sales manager katika kampuni fulani akaenda ofisin akaweka appointment na watu kumi kwa siku akaenda kuuza bidhaa ya mhindi na kwa nguvu kubwa anaona hapo amefanya kazi kubwa na ya maana sana, lakini huyu mtu hawezi kufikiria angeweza kununua same product na akafanya kama navyofanya kwa mhindi na akauza ile faida yote ikaingia kwa mfuko wake ye anachooni nikifanya hivi ni umachinga (akili finyu, ukosefu wa maarifa na kufikiri). Biashara hii ukiifanya kiutalaamu kama inavyotakiwa ni sehemu ya kujipatia milioni yako ya kwanza kwani utalipwa kutokana na juhudi zako na wala si kutokana na usingizi au position yako katika jamanii. Huku ni haki sawa, na ni kazi kama kazi nyingine Utaifanyaje biashara hii kiutaalama ni ukae chini uisome na uielewe ndio ufanye biashara, wengi tunaona tunapoteza muda wa kujifunza ndio maana tunabaki kutafuta kazi miaka miwili wakati ungeweza kujiattach na mtu na ukafanya kazi kama watu wengine ukajipatia kipato kama watu wengine huku ukiwa ni boss mwenyewe na hii itakuwezesha wewe kukuza uwezo wako wa kujiongoza na kuongoza wengine Kwa wale wanaofanya biashara hii kiutaalamu na kama mfumo wa biashara hii unavyotakiwa wao ndio wanaofaidi matunda ya biashara hii na ndio maana matajiri wengi ulimwenguni wakiwa katika mahojiano na vyombo vya habari akiulizwa ingekuwa ndio unaanza kutafuta maisha au kuanza biashara sasa hivi utafanya biashara gani? ,,,,, wanajibu with confidence kabisa nitaanza na biashara ya mtandao (Kiyosaki, Bill Gat,Randy Gage, steve job enzi za uhai wake) hii ni kwasababu ya mfumo wa biashara wenyewe, mfumo wa biashara hii unakufanya wewe unufaike na kazi unayoifanya na kujipatia hela ya kufanya uwekezaji na kuongeza kipata kwa ushirikiano na watu ( team work), huwezi kupata mafanikio bila watu. Kwenye mfumo huu wa biashara ndio sehemu pekee ambapo tayari ushaandaliwa mfumo wa biashara na plana ya biashara wewe kazi yako ni kufuata mfumo tuu. Ni kwa njia gani utafanya hii biashara kiutaalam na unufaike usikose kusoma post ijayo itakayo kueleza mfumo mzima wa jinsi ya kunufaika na kufanya biasharaa hii Mafanikio ni uyafuate wewe na hayawezi kukufuata,,,, ukitegemea jamii iaprove kazi unayoifanya utakufa njaa na mwisho umaskini utakuwa rafiki yako Ni kwa kujituma na kufanya vitu sahihi ndio siri ya mafanikio Kumbuka chochote kizuri kinabarikiwa na chenye uzuri ni adui wa kila mtu Kwa mawasiliano usikose kuniandikia kwa dorisulicky@gmail.com